POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendesha mafunzo kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wamiliki na madereva wa magari,pikipiki na bajaji ikiwa ni sehemu ya njia za kukabiliana na ajali zinazojitokeza na kusababisha vifo na majeruhi. 
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro yamefanyika leo Alhamis Julai 12,2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Shinyanga. 
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema suala la utii wa sheria za barabarani ni jukumu la watu wote hivyo kila mmoja lazima azingatie sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
"Madereva ni wadau wakuu wa kuzuia ajali za barabarani, nalipongeza jeshi la polisi kwa kuona umuhimu na wadau hawa ili kuwapa elimu hii kwani madereva wakisikiliza na kufanyia kazi elimu hii hakika ajali hazitatokea mkoani Shinyanga",alieleza Matiro.
"Ili kutokomeza ajali,ni vyema jeshi la polisi likaendelea kufanya doria katika barabara kuu, ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More