Polisi wa Texas waomba msamaha baada ya kumuongoza mtu mweusi kwa kumfunga kamba - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Polisi wa Texas waomba msamaha baada ya kumuongoza mtu mweusi kwa kumfunga kamba

Polisi wa Texas wameomba msamaha baada ya picha ya maafisa weupe wawili wakiwa wamepanda farasi wakiongoza mtu mweusi aliyeonekana amefungwa kwa kamba hatua iliyozusha ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.Mkuu wa Polisi wa Galveston, Vernon Hale alisema Jumatatu mbinu hiyo ilikuwa inakubalika katika baadhi ya matukio, lakini kwamba “maafisa hawakufanya uamuzi mzuri katika tukio hili”.


Alisema hakuna “nia mbaya” na imebadilisha sera ya idara “kuzuia utumiaji wa mbinu hii”.


Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wamesema picha hii imeibua mawazo kuhusu nyakati za utumwa.


Kulingana na habari iliyotolewa kutoka kwa Idara ya Polisi ya Galveston, maafisa hao wawili kwa majina P Brosch na A Smith, walimkamata Donald Neely baada ua kukiuka sheria.


Polisi walifafanua kwamba hakufungwa na kamba, lakini “alikuwa amefungwa pingu mikononi na kamba ilikuwa imefungwa kwenye pingu.


Idara iliongeza: “Tunaelewa maoni hasi kuhusu hatua hii na tunaamini maoni haya yanafaa kabisa kuk... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More