Polisi wala rushwa kutimuliwa kazi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Polisi wala rushwa kutimuliwa kazi

Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha
JESHI la Polisi mkoa wa Arusha,limesema kuwa litawafukuza askari wa jeshi hilo pamoja na maafisa wake bila kujali cheo chake ikiwa watabainika kuomba rushwa kutoka kwa madereva wa magari ya waongoza watalii pamoja na wamiliki wa makampuni hayo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shana ameyasema hayo kwenye kikao cha wadau wa utalii mkoa wa Arusha kilichofanyika kwenye hotel ya Gran Melia, jijini Arusha.kilichokuwa kikijadili changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.Akitoa salamu zake kwenye kikao hicho kilichoongozwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Costantini Kanyasu, Kamanda Shana amesema amepokea malalamiko ya baadhi ya askari kupokea rushwa .
Amesema kuwa ikithibitika askari ameomba rushwa kutoka kwa wamiliki wa makampuni ya waongoza utalii au madereva wa magari hayo atawafukuza mara moja na endapo kama atakuwa ni polisi mwenye nyota ataomba kibali kwa mamlaka husika cha kumfukuza afisa huyo.
Wakichangia kwenye kikao hicho wada... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More