POLISI WILAYA YA TABORA INAMSAKA ALIYESABABISHA TAHARUKI KWA KUTUMA MESEJI YA UONGO KUHUSU KUTEKWA WATOTO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI WILAYA YA TABORA INAMSAKA ALIYESABABISHA TAHARUKI KWA KUTUMA MESEJI YA UONGO KUHUSU KUTEKWA WATOTO

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
JESHI la Polisi Wilaya ya Tabora linaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza ujumbe wa uongo juu ya kutekwa wa wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi ChemChem uliosababisha taharuki kwa wananchi na kupelekea kuharibu mali za Polisi.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tabora (OCD) John Mfinanga wakati akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora kwenye kikao cha robo ya kwanza.Alisema ujumbe huo ulisababisha kuwepo na uvunjifu wa amani ambao ulitokana na baadhi ya raia kuanza kuwashambulia Polisi na mgari yao na kupelekea kupasuliwa vyoo.
Mfinanga alisema hadi leo ikiwa saa 30 zimeshapita hakuna mzazi aliyejitokeza kutoa taarifa juu ya kupotelewa na mtoto jambo linaonekana lilikuwa na uongo na lenye nia ya kuleta vurugu katika jamii.“Waheshimiwa Madiwani ni mzazi gani anaweza kukaa zaidi ya masaa 24 mtoto wake amepotea hatoi taarifa…tunamtafuta aliyesambaza meseji hiyo ili hatimaye tumfikishe anapostahili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More