POLISI YAKAMATA WATATU KUTEKWA KWA DEWJI, MAKONDA AAHIDI MO ATAPATIKANA AKIWA SALAMA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI YAKAMATA WATATU KUTEKWA KWA DEWJI, MAKONDA AAHIDI MO ATAPATIKANA AKIWA SALAMA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
JESHI la Polisi nchini linamtafuta mfanyabiashara Mohammed ‘Mo’ Dewji aliyetekwa mapema leo asubuhi akiwa anaingia katika gym ya Collesium eneo la Oysterbay mjini Dar es Salaam kufanya mazoezi.
Taarifa zinasema Mo Dewji mwenye umri wa miaka 43 alitekwa asubuhi ya leo akiwa anaingia kwenye gym hiyo kama ilivyo ada yake kila siku asubuhi kwa ajili ya mazoezi.
Watu wasiojulikana walifyatua bunduki hewani mfululizo wakati Dewji anateremka kwenye gari yake kabla ya kumbeba na kumpakia kwenye gari lao na kutokomea naye kwa kasi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutekwa kwa Mo Dewji na amesema Jeshi lake linawashikilia watu watatu juu ya sakata hilo, lakini amesema kwamba kamera za CCTV hazioneshi vizuri sehemu ambayo watekaji waliingilia.

Mohammed ‘Mo’ Dewji ameetekwa leo asubuhi akiwa anaingia katika gym ya Collessium eneo la Oysterbay mjini Dar es Salaam kufanya mazoezi 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More