POPADIC KOCHA MPYA SINGIDA UNITED, MSAIDIZI WAKE MSERBIA PIA, DUSAN - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POPADIC KOCHA MPYA SINGIDA UNITED, MSAIDIZI WAKE MSERBIA PIA, DUSAN

Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
WALIOWAHI kuwa makocha wa Simba SC kwa wakati tofauti, Dragan Popadic na Dusan Momcilovic wamejiunga na klabu ya Singida United.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Singida United imewatambulisha makocha hao wawili raia wa Serbia ikisema Popadic atakuwa kocha mkuu na Msaidizi wake, Momcilovic.   
Popadic alipata umaarufu mkubwa wakati akiifundisha klabu ya SImba SC kati ya mwaka 1994 na 1996 kabla ya kuondoka, wakati Momcilovic alikuwa Msaidizi wa kocha Muingereza, Dulan Kerr katika klabu hiyo mwaka kati ya mwaka 2015 na 2016.
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo akimtambulisha kocha mpya, Dragan Popadc (kushoto). Kulia ni Dusan Momcilovic


Wakati Popadic ni mwalimu kamili na aliyebobea katika soka ya Afrika, Momcilovic ni kocha wa mazoezi ya viungo wa kiwango cha juu pia.
Singida United inaajiri Waserbia hao kiasi cha miezi saba tangu iachane na kocha wake Mholanzi, Hans van der Pluijm aliyehamia Azam FC.
Ikumbukwe baada ya kuondoka Pluijm ambaye walimch... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More