Posta mnawajibu wa kurahisisha utoaji wa huduma kidigitali -Dkt.Yonazi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Posta mnawajibu wa kurahisisha utoaji wa huduma kidigitali -Dkt.Yonazi

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa Shirika la Posta Tanzania linawajibu wa kuisaidia Serikali katika kuharakisha maendeleo kwa kurahisisha utoaji wa huduma za barua, nyaraka, vipeto na vifurushi ndani na nje ya nchi kwa kwenda kidigitali ambako dunia ndio iko huko. duma
Hayo ameyasema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano -Mawasiliano Dkt.Jimmy Yonazi wakati alipomwakilisha Waziri wa Wizara hiyo katika siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 145 ya Umoja wa Posta duniani.
Dkt. Yonazi amesema kuwa shirika hilo limekuwa likirahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha za uwakala hasa maeneo ambayo hayafikiwi kirahisi na Kampuni pamoja na taasisi zinazotoa huduma za kibiashara.
Dkt. Yonazi amesema shirika linajukumu la msingi la kutoa huduma za posta kwa watu wote hivyo ni muhimu likaendelea kuboresha mikakati yao ili liweze kuwafikia watanzania kote nchini ikienda sambamba na huduma bora.
"Tupo Serikali ya awam... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More