PPRA wapeta kidigitali: Wahandisi wapewa fursa za ununuzi kwa njia ya mtandao - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PPRA wapeta kidigitali: Wahandisi wapewa fursa za ununuzi kwa njia ya mtandao

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imeendelea kuwapa wadau wake elimu na ufafanuzi kuhusu fursa na faida za kutumia mfumo wa ununuzi wa njia ya mtandao (TANePS).

Afisa Tehama wa PPRA, Giftness David, akijibu maswali ya wahandisi kuhusu TANePS


Mamlaka hiyo imetumia fursa ya maonesho ya mkutano wa 16 wa mwaka wa Wahandisi yaliyoandaliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), yaliyofanyika Septemba 5 hadi 7 jijini Dar es Salaam.


Pamoja na mambo mengine, PPRA ilikuwa inapokea maoni na kujibu maswali mbalimbali yaliyohusu mfumo wa ununzi kwa njia ya mtandao (TANePS) pamoja na masuala yanayohusu marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma yaliyofanyika mwaka 2016.


Katika maboresho ya sheria ya ununuzi wa umma, wahandisi walijikita zaidi katika marekebisho ya kanununi Na. 55A, 55B, 55C NA 55D, kama walivyoelezwa na mgeni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kuwa kupitia maboresho ya sheria ni vyema wakachangamkia fursa za miradi ya serikali kuliko kulalamika kila wakati kuwa wanakosa... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More