Prof. Lipumba ashinda kwa kishindo Uenyekiti CUF, hatma ya Maalim Seif ipo mikononi mwake - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Prof. Lipumba ashinda kwa kishindo Uenyekiti CUF, hatma ya Maalim Seif ipo mikononi mwake

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahm Lipumba amefanikiwa kutetea nafasi yake hiyo kwa mara ya tano, baada ya kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika jana, ambapo alikabiliwa na washindani wengine wawili.

Related imageProf. Lipumba

Washindani waliojitokeza dhidi yake ni pamoja na Mwenyekiti Wanawake wa CUF tawi la Ubungo jijini Dar es Salaam, Diana Daudi Simba na aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Arusha Mjini mwaka 2015 kwa tiketi ya CUF ambaye pia ni Katibu wa CUF mkoani Arusha, Zuberi Mwinyi Hamisi.

Katika uchaguzi huo wa mwaka 2015 huko Arusha, Zuberi alipata kura 106, wakati mshindi alikuwa Godbless Lema wa Chadema aliyepata kura 68,868. Katika uchaguzi wa jana, Lipumba alichaguliwa kwa kura 516 sawa na asilimia 88.9, Zuberi alipata kura 36 sawa na asilimia 6.2 huku Diana akipata kura 16 ambazo ni sawa na asilimia 2.8. Kura za jumla zilizopigwa ni 598.

Kwa ushindi huo wa kishindo, Prof. Lipumba atakiongoza tena chama hicho kwa miaka mingine mitano h... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More