PROF. MDOE: WANAFUNZI 124,000 KUNUFAIKA NA MKOPO WA ELIMU YA JUU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PROF. MDOE: WANAFUNZI 124,000 KUNUFAIKA NA MKOPO WA ELIMU YA JUU

Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiMAOFISA wanaosimamia madawati ya mikopo vyuoni wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora isiyokuwa na urasimu na badala yake wahakikishe wanaimarisha madawati hayo ili kuhakikisha wanafunzi wenye sifa na uhitaji wanufaika na mikopo kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe wakati akizungumza katika kikao kazi cha siku mbili cha maafisa hao kilichoanza mjini Bagamoyo.
Amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata Elimu ya juu bila kikwazo.
Profesa Mdoe amesema kwa mwaka wa fedha 2018/19 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 427. 5 ambapo jumla ya wanafunzi 124 watanufaika na mkopo huo, na kuwa ugawaji wa mikopo hiyo uzingatie haki, vigezo, kanuni na sheria.
“Nataka twende vizuri tukahakikishe huduma bora inatolewa katika mwaka huu mpya wa masomo ikiwa ni pamoja kutoa huduma ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More