PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTSPESA YAZINDULIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTSPESA YAZINDULIWA

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya  kubashiri michezo nchini ya Sportspesa imezindua rasmi promosheni ya kuinua watu maisha yao hasa kiuchumi inayokwenda kwa jina la Shinda zaidi na Sportspesa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Tarimba Abbas amesema kampuni hiyo inaendesha shindano hilo kwa wateja wake ikiwa ni mara ya pili.

Ambapo kwa mwaka jana ilitoa takribani bajaj 100 kwa washindi kutoka mikoa mbalimbali nchini waliobuka washindi.

Pia Tarimba amesema  lengo la shindano hilo limejikita zaidi kwenye kubadilisha maisha ya Watanzania kwani washindi wamekua wakishinda zawadi mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingne zinawasaidia kujiongea kipato.

Ametoa rai kwa wateja kutumia fursa hiyo kubadilisha maisha yao kwani promosheni hiyo kila mmoja anayo nafasi ya kuwa mshindi na kufafanua shindano hilo linaambatana sana na wapenzi wa mpira wa miguu.

Kwa upande wa Submean Auto Limited Venkatesh Bussiness ambao ni... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More