Pumzi ya Barcelona kwenye mapafu ya Hazard na Alcantara - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Pumzi ya Barcelona kwenye mapafu ya Hazard na Alcantara

Kuna tofauti kubwa ya usajili na makelele ya Mitandaoni na majarida ya wanaochumia tumbo.

Ukiangalia Barcelona inahitaji mabadiliko makubwa mno. Na mabadiliko hayo yanapaswa kuwa yenye tija na ufundi ndani yake.


Bila shaka usajili wa Ousmane Dembele niliona ni usajili wa kupanic kama ule wa David Beckham kwenda Real Madrid. Madrid walimkosa Ronaldinho wakamua kumnunua Beckham, tena kwa stresi wakamuuza makelele. Madrid wakamkosa Neymar wakamkimbilia Bale.Barcelona walipompoteza Neymar walishikwa na kiwewe. Huu ni wakati wa wao kutulia. Hawapaswi kuiga kinachofanyika na Madrid. Kuna uwezekano mkubwa Madrid ikatumia pesa nyingi. Tena huenda wale wachezaji wanaohitajika na Barcelona wakawindwa kwa gharama kubwa.


Barcelona wanapaswa kutumia mwanya wa tumbo joto la Perez kununua wachezaji kwa kuangalia kiu yao wala sio ushindani. Madrid huenda wakapanic tema wakanunua wachezaji kwa hela kubwa mno.


Barcelona kuna uwezekano mkubwa wa kufanya biashara kiurahisi sana kama watatulia. Kwanza wamruhusu Rakitic kuondoka. Ujio wa Athur una tija. Rakitic akienda wamrudishe Thiago Alcantara kuja kuziba pengo la Xavi. Nafasi ya Iniesta bila shaka itachukuliwa na Coutinho.Nimesikia taarifa za Hazard kwenda Barcelona. Huu utakuwa usajili bora kwao. Utakuwa usajili bora kwa miaka 20 iliyopita tokea wampate Ronaldinho. Upande wa kushoto wa Barcelona unahitaji mtu mwenye kasi kama Iniesta. Kuna jambo moja la kufanya. Chelsea hawawezi kumkataa Rakitic kwa sababu Bakayoko amefeli. Hawana mbadala sahihi wa Matic. Sioni chumba cha Drinkwater. Kama watapewa dau nono na mchezaji kama Denis Suarez na Rakitic sidhana kama watakataa ofa hii. Na pia sidhani kama Hazard anaweza kugoma kwenda Barcelona.


Takwimu za Eden Hazard
Kuzaliwa Jan 7, 1991 (27), Kimo: 1,73 m

Mkataba: 30.06.2020

Eden Hazard

Thamaini

110,00 Mill. €


Takwimu

Kiungo89%Mashindano Mechi G A Y Y&R R dkk
Jumla 495 139 128 26 1 36.910′
Premier League Premier League 208 69 46 13 16.542′
Ligue 1 Ligue 1 147 36 41 8 10.277′
UEFA Champions League Champions League 44 8 13 2 3.468′
Europa League Europa League 23 3 6 1 1.490′
FA Cup FA Cup 21 5 9 1 1.436′
EFL Cup EFL Cup 20 5 6 1 1 1.193′
Coupe de France Coupe de France 13 6 2 1.047′
Coupe de la Ligue Coupe de la Ligue 6 3 2 493′
Europa League Qualifiers Europa League Qualifiers 5 2 1 272′
FIFA Club World Cup Club World Cup 2 1 176′
UEFA Supercup UEFA Supercup 2 1 202′
Community Shield Community Shield 2 160′
Trophée des Champions Trophée des Champions 1 1 1 80′
Premier League 2 Premier League 2 1 774′

Hazard hapaswi kuogopa kucheza na Messi eti kisa atacheza chini ya kivuli chake. Hapana. Hizo ni siasa za kijinga zilizomponza Neymar. Neymar alihitaji mkwanja mrefu wala hakuondoka Barcelona eti kisa yupo chini ya kivuli cha Messi.Aliyemdanganya Neymar kwamba anaweza kushindana na Messi ni nani? Kabla hujawaza kumzidi Messi fikiria kwanza kuhusu Ribery kumshindwa Ronaldo. Ina maana Neymar anataka kutufanya wazembe wa kufikiria kiasi hiki? Yaani Iniesta na Sneijder walishindwa kabisa kumtoa Messi kwenye kinyang’amyiro cha BDO ndio aje kuwa yeye!Hata hivyo huyo Hazard hata kama ataenda Madrid hawezi kumzidi Messi au kushindana nae.


Kama dili la Hazard litakwama nawasilisha hoja kwamba Willian pia atawafaa
P KU Dkk G A K S YC RC


Willian36 20 1883 6 7 25 54 2 0
Dembele 17 12 930 3 6 10 21 2 0

P-Mechi, KU-Mechi alizoanza, G-Goli, A-Asisti, K-Kulenga golini, S-Idadi ya mashuti, Y-Njano, R-Nyekundu


Ukitaka kujua Dembele ni aina ya akina Zaha, hakuna timu ambayo inaweza kutoa zaidi ya Euro Mil 120 kumtaka Dembele kwa sasa. Kuna mambo mawili ya kufanya hapa. Aidha wafanyr mazungumzo na Bayern wamwachie Dembele na fedha kidogo ili wamnase Thiago. Bayern inahitaji mawinga. Roben na Ribery umri umeenda kidogo wanaweza kusikiliza hili dili. Au wakae chini na Chelsea wajua watasaidana vipi kwenye suala la Wilian.Chelsea wanaweza kulipa fadhila kwani wao Barcelona waliwapa Pedro na Fabregas. Ni namna tu ya kuwabembeleza. Willian anampenda sana Ronaldinho lakini anamheshimu Messi na aliwahi kuweka wazi hilo.


Dybala na Griezmann mhh sidhani kama wanaweza kupatikana. Griezmann kaongeza mkataba na Dybala na Messi sidhani kama wana mahusiano Mazuri. Tumeona timu ya taifa Dybala kasuswa kabisa. Kama Messi angekuwa na maelewano mazuri sidhani kama amhekubaliana na uamuzi wa mwalimu kumweka benchi.Nimeshangaa sana Barcelona kukaa kimya dili la Jack Wilishere na Riyadh Mahrez. hawa ni wachezaji waliokuwa wanawafaa kabisa Barcelona. Hata Juan Mata ni moja ya wachezaji wepesi sana na wenye aina ya uchezaji kama wa Barcelona.


P KU Dkk G A K S YC RC


Willshere20 12 1187 1 3 5 15 6 0


Mahrez36 34 2090 12 10 36 73 2 0


Rakitic35 31 2860 1 5 11 28 4 0

Yaan Rakitic kamzidi Wilshere michezo 15 lakini ana bao moja sawa na Wilshere na kumzidi asisti mbili tu. Tena akiwa Barcelona wakati mwenzake yupo Arsenal. Hii ndio sababu kubwa ya mimi kuamini kwamba Rakitic ameshindwa kuvaa viatu vya Xavi. Ericksen angewafaa lakini sidhani Tottenham watamwachia.


Wanahitaji usajili usajili wa watu wawili tu sasa


Rakitic=Willian/Hazard


Dembele=Thiago


Makala na Privaldinho (Instagram)


Source: Shaffih DaudaRead More