PUMZIKA KWA AMANI AMRI ATHUMAN 'KINGI MAJUTO' - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PUMZIKA KWA AMANI AMRI ATHUMAN 'KINGI MAJUTO'

Msanii wa vichekesho nchini Amri Athuman maarufu King Majuto, amefariki leo Jumatano Agosti 8, 2018 saa mbili kamili usiku katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alilazwa tangu tarehe 31 Julai, 2018.
Taarifa za msiba huo wa nguli wa maigizo zimethibitishwa na Afisa habari wa Muhimbili Aminiel Eligaisha ambapo amesema Mzee Majuto amefariki akiwa anaendelea na matibabu ambayo aliyaanza Julai 31, mwaka huu baada ya jitihada za madaktari kuokoa uhai wake kushindikana.
''Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa mbili alikata roho'', amesema.
Mzee Majuto alianza kuumwa muda mrefu akisumbuliwa na tatizo la nyonga ambapo mapema mwezi Mei alipelekwa nchini India kwaajili ya matibabu kabla ya kurejea nchini mwezi Juni ambapo alifikia Muhimbili lakini baadae alipata nafuu na kwenda nyumbani kabla ya... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More