PWANI YATILIANA SAINI MKATABA WA USAMBAZAJI DAWA ,VIFAA TIBA KUPITIA MSHITIRI MMOJA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PWANI YATILIANA SAINI MKATABA WA USAMBAZAJI DAWA ,VIFAA TIBA KUPITIA MSHITIRI MMOJA

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 
MKOA wa Pwani,umefikia asilimia 90 ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ,hadi kufikia octoba 2018, hatua ambayo inaelekea kwenda kupunguza kero ya upungufu wa dawa na vifaa hivyo kwenye vituo vya afya.

Hayo yalibainika ,wakati wa kikao cha mkoa cha zoezi la kusaini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),zoezi ambalo limefanywa baina ya katibu tawala wa mkoa Theresia Mbando na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha.

“Kwa mujibu wa taarifa zinavyotolewa katika mfumo wa kukusanya na kuchambua data za afya (DHIS 2 ),hadi kufikia kipindi hicho wamefikia asilimia hiyo jambo ambalo limenifurahisha” alisema Theresia . Theresia alisema ,kwa hatua waliyofikia mzabuni huyo anatarajiwa atafikisha lengo la upatikanaji wa dawa kwenye vituo na halmashauri za mkoa kwa asilimia 100.

“Wananchi wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyetu hivyo ni imani... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More