RAIA WA INDIA AFIKISHWA KORTINI AKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIA WA INDIA AFIKISHWA KORTINI AKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
 RAIA wa India ambaye ni meneja wa tawi la kampuni ya Neelkani Salt Limited, Mohammed Alikhan (29) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili.
Katika kesi hiyo namba 114 ya mwaka huu, mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji wa fedha na wizi wa katoni za chumvi 45,919 zenye thamani ya Sh413, 559,000/_
Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega kuwa kati ya Januari Mosi, 2018 na Julai 29, mwaka huu katika mtaa wa Arusha Ilala, Jijini Dar Es Salaam, Alikhan akiwa Meneja wa tawi la kampuni hiyo aliiba katoni za chumvi 45,871 aina ya Neel Mali ya mwajiri wake zenye thamani ya Sh 412,839,000.
Pia mshtakiwa huyo anadaiwa katika kipindi hicho aliiba kilo moja ya chumvi aina ya Neel Gold yenye thamani ya Sh 720,000. Mshtakiwa huyo anadaiwa pia kuiba jumla ya chumvi 45,919 zenye thamani ya Sh 413,559,000.
A... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More