RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA JELA MIAKA 20 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA JELA MIAKA 20

Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii
MKURUGENZI wa Fairme NGO, Rene Staheli (62) ambaye pia ni raia wa Uswis leo Oktoba 23, 2018 amehukumiwa kulipa faini ya Sh Sh. Milioni 34 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kukiri kosa la kukutwa na vipande vitatu vya meno ya Kiboko.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Rwizile amesema mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kufuatia yeye mwenyewe kukiri kosa lake.
Kufuatia kukiri kutenda kosa linalokukabiki na kukubali vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapa,mahakama inakutia hatiani na inakuhukumu kulipa faini ya Sh 34,036,188 na iwapo utashindwa basi utatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani", amesema Hakimu Rwizile.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita aliiomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshtakiwa huyo kwa kukutwa na maliasili yetu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.Katika utete... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More