RAIS DK MAGUFULI, MSTAAFU DK KIKWETE WAUAGA MWILI WA MSANII KING MAJUTO LEO DAR - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS DK MAGUFULI, MSTAAFU DK KIKWETE WAUAGA MWILI WA MSANII KING MAJUTO LEO DAR

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete wameshiriki zoezi la kuuaga mwili wa msanii wa vichekesho marehemu Amri Athumani ‘King Majuto’ katika ukumbi wa Karimjee mjini Dar es Salaam. 
Ibada ya kuusalia mwili wa marehemu King Majuto imeongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakari Zubeiry ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam. 
Marehemu King Majuto ameagwa leo na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao mkoani Tanga kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho nyumbani kwake, Tanga.
King Majuto amefariki dunia Saa 1:30 usiku wa jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili mjini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa matibabu kufuatia hali yake kubadilika na kuwa mbaya wiki iliyopita.
Dk. John Pombe Magufuli akisoma dua zake mbele ya mwili wa msanii wa vichekesho, marehemu Amri Athumani ‘King Majuto’ leo ukumbi wa Karimjee mjini Dar es Salaam. 

Rais Dk. John Pom... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More