RAIS DKT MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE KWA KUKABIDHI MATREKTA 10 KWA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE (SUA) CHA MOROGORO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS DKT MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE KWA KUKABIDHI MATREKTA 10 KWA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE (SUA) CHA MOROGORO

Na Sultani Kipingo, KibahaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kutoa matrekta 10 kwa Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kuimarisha utoaji wa mafunzo ya kilimo na kuzalisha wataalamu bora wa kilimo nchini.Matrekta hayo 10 aina ya Ursus yamekabidhiwa Jumamosi Agosti 11, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James huko Kibaha Mkoani Pwani na kueleza kuwa SUA imepatiwa matrekta hayo ikiwa ni juhudi za Serikali za kuendeleza kilimo ambacho kinatoa ajira kwa watanzania wengi.Matrekta hayo yana thamani ya Shilingi Milioni 587.5Bw. Doto James amekitaka Chuo Kikuu cha SUA kuyatumia matrekta hayo vizuri na kwamba Serikali itafuatilia kupitia kitengo cha Wizara ya Fedha na Mipango cha kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo katika taasisi ambayo inapokea fedha za Serikali.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SUA Prof. Yonika Ngaga amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi hiyo pamoja na kutekeleza ah... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More