RAIS DKT MAGUFULI ATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA VIFO VYA WAFANYAKAZI WA AZAM TV - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS DKT MAGUFULI ATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA VIFO VYA WAFANYAKAZI WA AZAM TV

Watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori leo asubuhi Jumatatu Julai 8, 2019 katika eneo la Malendi wilayani Iramba mkoani Singida.
Inaelezwa kuwa walikuwa wakieleleka wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi unaofanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia.
Waliofariki dunia watano ni wafanyakazi wa Azam TV na madereva wawili wa gari ya kukodi ambao majina yao bado hayajafahamika.
Wafanyakazi wa Azam Tv waliofariki dunia ni: 

Said Haji - Camera manCharles Wandwi -Camera manSalim Mhando - Switcher Florance Ndibalema- SoundSylvanus Kasongo - Engineer 
MajeruhiMohamed Mwinshehe Mohamed MaindeArtus Massawe 
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Igunga Merichad Magon... Continue reading ->Source: KajunasonRead More