RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa uchumi wa Zanzibar umeendelea kuimarika sambamba na ukusanyaji mzuri wa mapato na matumizi yake.

Hayo aliyasema leo, katika ukumbi wa Ikulu ndogo Kibweni mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa Kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Wizara hiyo ya Fedha na Mipango kwa kuendelea kusimamia vyema kuimarika kwa uchumi wa Zanzibar pamoja na mapato na matumizi yanayofanyika.

Alieleza kuwa katika ukusanyaji wa mapato licha ya udogo wake Zanzibar lakini inaonekana ni jinsi gani ilivyopiga hatua na kuweza kupata mafanikio makubwa yanayoonekana.

Hata hiyo, Rais Dk. Shein Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi na watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kushirikiana kwa pamoja na kusaidia sambamba na kuaminiana ili maf... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More