Rais Donald Trump amkosoa Rais wa Ufaransa Macron kuhusu pendekezo lake la kuundwa kwa jeshi la Umoja wa Ulaya - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Donald Trump amkosoa Rais wa Ufaransa Macron kuhusu pendekezo lake la kuundwa kwa jeshi la Umoja wa Ulaya

Rais wa Marekani Donald Trump hakupoteza muda kumkosoa mwenyeji wake wa Ufaransa wakati alipowasili Paris kwa ajili ya matukio ya kuadhimisha kumbukumbuku ya miaka 100 ya kumalizika Vita Vikuu Vya Kwanza vya Dunia. Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wakati alitua Paris, akisema kuwa Rais Emmanuel Macron ametoa pendekezo aliloliita kuwa ni “matusi” la kuunda jeshi la Ulaya ili kupambana na Marekani, China na Urusi.Ilikuwa dalili ya wazi kuwa rais huyo anayeendeleza sera ya “Marekani Kwanza” yuko tayari kuufuata mkondo wake kwa mara nyingine tena wakati viongozi wa dunia wakikutana kukumbuka muungano ulioweka kikomo vita vya kwanza vya dunia.Kwa mujibu wa DW Swahili, Trump anapanga kukutana na Macron Jumamosi kwa mazungumzo kuhusu mada tofauti yanayotarajiwa kujumuisha usalama wa Ulaya, Syria na Iran. Wakati aliwasili, Trump aliandika kwenye Twitter kuwa Macron “amependekeza kuwa Ulaya iunde jeshi lake ili kujilinda dhidi ya Marekani, China na Urusi... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More