Rais Magufuli afanya uteuzi mdogo, Waziri Kairuki ahamishwa Wizara (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli afanya uteuzi mdogo, Waziri Kairuki ahamishwa Wizara (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuteua Mawaziri, Makatibu wakuu na Balozi.Kwenye mabadiliko hayo, aliyekuwa Waziri wa Madini Mhe. Angela Kairuki amehamishwa na kuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu / Uwekezaji.

TAZAMA ORODHA KAMILI HAPA CHINI:

Angela Kairuki – Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/Uwekezaji
Dotto Biteko – Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo – Naibu Waziri Madini

Joseph Nyamhanga – Katibu Mkuu TAMISEMI

Zainabu Chaula – Katibu Mkuu Afya

Elius Mwakalinga – Katibu Mkuu Ujenzi

Doroth Mwaluko – Katibu Mkuu Sera

Doroth Gwajima – Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI

Francis K Michael – Naibu Katibu Mkuu UTUMISHI

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amefungua Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba ambao utakuwa katika mji wa Havana, na Balozi wake atatangazwa hivi karibuni.


The post Rais Magufuli afanya uteuzi mdogo, Waziri Kairuki ah... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More