Rais Magufuli Akiri Kuguswa na Kifo Cha Mzee Majuto - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli Akiri Kuguswa na Kifo Cha Mzee Majuto

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joh Pombe Magufuli amefunguka kuguswa na Kifo Cha mchekeshaji maarufu Mzee Majuto kilichotokea siku ya jana.


Rais Magufuli Martina barua ya Rambi Rambi kwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo DKT. Harrison Mwakyembe na kumtaka afikishe salamu hizo kwa Familia ya Mzee Majuto.


Katika salamu hizo Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Mwakyembe kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya Marehemu, Wasanii wote nchini, wadau wa sanaa, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha King Majuto.King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake”.
The post Rais Magufuli Akiri Kuguswa na Kifo Cha Mzee Majuto appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More