Rais Magufuli alitaka baraza la wadhamini la CCM kufanya tathmini ya mali za CCM - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli alitaka baraza la wadhamini la CCM kufanya tathmini ya mali za CCM


Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amelitaka Baraza jipya la wadhamini la chama hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mali za chama na jumuiya zake
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Julai 13, 2018 alipokutana na wajumbe wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema baraza hilo linapaswa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ambayo ni kusimamia mali zote za chama na jumuiya zake, kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mali za CCM na jumuiya zake, kutoa ushauri juu ya mabadiliko yoyote yanayohitajika katika umiliki wa mali.
Mwenyekiti huyo amesema pamoja na kutekeleza majukumu mengine ambayo yatakabidhiwa kwake na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Rais Magufuli amesisitiza hatarajii kuona dosari za usimamizi wa mali za chama zikiendelea na amewataka wajumbe hao kuhakikisha CCM inanufaika na mali zake na kuachana na utegemezi ambao umekuwa ukisababisha k... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More