RAIS MAGUFULI AMLILIA KING MAJUTO, ASEMA ALIKUWA KIELELEZO CHA SAFARI NDEFU YA SANAA KATIKA NCHI YETU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS MAGUFULI AMLILIA KING MAJUTO, ASEMA ALIKUWA KIELELEZO CHA SAFARI NDEFU YA SANAA KATIKA NCHI YETU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha msanii nguli wa filamu, maigizo na uchekeshaji Tanzania, Amri Athumani maarufu kama King Majuto.
Katika salamu zake kufuatia msiba huo wa usiku wa jana, Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo.
“King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake," amesema Rais Magufuli.
Rais Dk John Magufuli (kulia) alikwenda kumjulia hali King Majuto Januari 31 mwaka huu Mu... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More