Rais Magufuli amshawishi hadharani Mbunge wa CHADEMA ahamie CCM ‘hiki ni chama chenye upendo hakina ubaguzi’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli amshawishi hadharani Mbunge wa CHADEMA ahamie CCM ‘hiki ni chama chenye upendo hakina ubaguzi’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama chenye upendo na hakina ubaguzi katika kuwatumikia Watanzania, huku akimwagia sifa Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Ester Matiko kuwa anamuonekano wa CHADEMA lakini moyo wake ni CCM.


Image result for Rais Magufuli ccmMhe. Dkt. John Magufuli

Rais Magufuli amesema hayo leo Septemba 7, 2018 mjini Tarime wakati akihutubia wananchi wa wilaya hiyo kwenye ziara yake ya kikazi kanda ya ziwa.


Tarime ipo miongoni mwa miji 27, tumekopa mikopo nafuu kutoka India zaidi ya Trilioni 1.2 fedha hizi tukaamua tutapeleka kwenye mji gani?  hatukuubagua mji wa Tarime. Tarime walichagua wapinzani sehemu zote mbili lakini hatukubagua kwa sababu sababu wapinzani wanahitaji, CCM wanahitaji maji hata wale wasio na maji wanahitaji maji. Tumeupangia mji wa Tarime bilioni 14 katika miji 27 sikupeleka hata Chato nilikozaliwa pamoja na kwamba wanamatatizo na maji na waliichagua CCM.“amesema Rais Magufuli na kumshawishi Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Matiko kwa kumwambia hata akihamia leo CCM atapokelewa.


Nimeleta maji hapa Tarime ili watu wa Tarime wajue ukweli, ili hata Mhe. Matiko ajue ukweli, kwanza hata ukimuona usoni sura yake ni CHADEMA lakini kwenye moyo ni CCM, CCM tu. Kwa hiyo hata ukiamua siku nyingine unahamia CCM kama wenzako tutakupokea tu, tutafanyaje,“amesema Rais Magufuli kwa kumalizia kuzungumzia mradi mkubwa wa maji wilayani humo uliotekelezwa chini ya serikali yake ya awamu ya tano.


Kwa upande mwingine, Rais Magufuli ameeleza kuwa yeye ni mtu mwenye upendo na hofu ya Mungu na ameahidi kuwatumikia Watanzania wote wanaompenda na wasiompenda.


The post Rais Magufuli amshawishi hadharani Mbunge wa CHADEMA ahamie CCM ‘hiki ni chama chenye upendo hakina ubaguzi’ appeared first on Bongo5.com.


Source: Bongo5Read More