Rais Magufuli amtumbua Waziri wa Kilimo - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli amtumbua Waziri wa Kilimo

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeelezea mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, ambapo Rais Magufuli ametengua na kuteua waziri mpya pamoja na kumbadili Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)


Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa, Rais Dk John Magufuli, amemteua Innocent Bashungwa, kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, akichukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amesema Rais Magufuli amemteua Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akichukua nafasi ya Charles Kichere.


Kadhalika Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe akichukua nafasi ya Erick Shitindi ambaye amestaafu.

Aidha kabla uteuzi waziri mpya wa viwanda na Biashara Innocent Bashungwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.


Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Edwin Mh... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More