RAIS MAGUFULI AMUAGIZA DK. JINGU KUSIMAMIA UTENDAJI KAZI WA NGOs - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS MAGUFULI AMUAGIZA DK. JINGU KUSIMAMIA UTENDAJI KAZI WA NGOs

 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akipokea ua kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bi. Magreth Mussai wakati alipowasili katika Oifisi za Wizara mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu (kulia) akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.  Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akitoa shukurani kwa niaba ya Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 
Na Mwandishi Wetu DodomaRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Njingu kusimamia kwa karibu Usajili na Uratibu wa NGOs nchini kwani kumekuwa na vitendo vya ovyo vinavyofanywa na NGOs.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu ya Chamwino Dodoma wakati akiwaapisha viongozi watatu aliowateua hivi karibuni akiwemo Mkurugenzi wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Balozi Dkt Azizi Malima .Dkt Magufuli amesisitiza kuwa NGOs zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ambazo pamoja na mambo mengine zinayataka kuendesha shughuli  zao kwa uwazi hususani katika masuala ya mapato na matumizi ya fedha za ufadhili wa shughuli zake. “Nataka ukasimamie Usajili na Uratibu wa NGOs najua zipo chini ya Maendeleo ya Jamii kasimamie kuwe na uwazi wa utendaji kazi wa NGOs” alisisitiza Rais Magufuli.Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu amemuhakikishia Rais Magufuli kutekeleza majukuu yake kwa akili, moyo na nguvu zake zote ili kufikia mafanikio anayoyatarajiwa na yanayotarajiwa na watanzania.“Nikuahidi Mhe. Rais nitafanya kazi kwa nguvu na akili zangu zote kwa kushirikiana na wenzangu katika Wizara ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana”alisema Dkt. Jingu.


Source: Issa MichuziRead More