Rais Magufuli amuapisha Dk Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi nchini Canada - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli amuapisha Dk Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi nchini Canada

Rais Dk. John Magufuli leo amemuapisha Dk Mpoki Ulisubisya, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada.


Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya anakwenda kuchukua nafasi ya Aphayo Kidata aliyevuliwa ubalozi, huku sababu za kuvuliwa nafasi hiyo zikiwa bado hazijawekwa bayana. 


Dk Ulisubisya aliyeteuliwa kuwa balozi Janauri 9, 2019, ameapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam, na  katika hafla hiyo imeweza kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.


Kabla ya uteuzi huo Dk Ulisubisya alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia afya na nafasi yake ilichukuliwa na Dk Zainabu Chaula.Tweet... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More