Rais Magufuli atoa salamu za rambirambi ‘Mzee Majuto alikuwa kielelezo cha sanaa ya Tanzania’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli atoa salamu za rambirambi ‘Mzee Majuto alikuwa kielelezo cha sanaa ya Tanzania’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha msanii mkongwe hapa nchini Mzee Amri Athuman maarufu kwa jina la King Majuto kilichotokea tarehe 08 Agosti, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli walipomtembelea ili kumjulia hali msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam Januari 31, 2018


King Majuto amefariki dunia majira ya saa 1:30 Jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.


Katika salamu hizo Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Mwakyembe kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya Marehemu, Wasanii wote nchini, wadau wa sanaa, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha King Majuto.


Mhe. Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More