Rais Magufuli Kuongoza Mkutano Mkubwa wa Kisiasa Duniani Unaoratibiwa na Chama cha kikomunisti cha China (CPC) - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli Kuongoza Mkutano Mkubwa wa Kisiasa Duniani Unaoratibiwa na Chama cha kikomunisti cha China (CPC)


Rais  John Magufuli anatarajiwa kuongoza mkutano wa vyama vya siasa vyenye mlengo wa kijamaa utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17, mwaka huu.
Mkutano huo pia utashirikisha viongozi wa mataifa mbalimbali akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi ambaye atawakilisha Chama cha kikomunisti cha nchi hiyo (CPC).
Wengine watakaoshiriki katika mkutano huo ni viongozi wa vyama vilivyopigania uhuru na ukombozi wa Bara la Afrika na Kusini mwa bara hilo, vikiwamo vyama vya Frelimo, ANC ,ZANU PF na vinginevyo.
Mkutano huo ni wa pili kufanyika Duniani, ambapo wa kwanza ulifanyika Beijing, China Desemba mwaka jana, ambapo Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping alihudhuria na kuziasa nchi za Afrika kuleta maendeleo.
China ni miongoni mwa nchi zilizo mstari wa mbele kusaidia nchi za Afrika ikiwamo Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizo zinapiga hatua za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii, hali ambayo inaweza kuwasaidia kuondoka kwenye utegemezi.
Miongoni m... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More