Rais Magufuli Mgeni Rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri Bonde la Mto Nile - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Magufuli Mgeni Rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri Bonde la Mto Nile

Jonas Kamaleki, MAELEZO, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuri atakuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Bonde la Mto Nile zilizopo kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maji, Prof. Makae Mbarawa amesema Mkutano huo utapitia utekelezaji masuala mbali mbali ya miradi, utapokea taarifa ya utendaji, hali ya ulipaji wa michango ya kila mwaka kwa nchi wananchama na tathmini ya watumishi wa Sekretarieti ya NELSAP.
Mkutano huo ambao utafanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2018 utawashirikisha mawaziri wa Maji na wawakilishi kuto nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani ya Kusini na Uganda.Prof. Mbarawa amesema kuwa Mkutano huu utatanguliwa na vikao vya wataalamu ambavyo ni vya kiutendaji na vitaanza tarehe 20 hadi 21 Novemba, 2018 Jijini Dar es Salaam.
“Ushirikiano wa Nchi za Bonde la Mto Nile ni wa muda mrefu, um... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More