Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aongoza Kikao kazi cha Shirikisho za Kiuchumi za Afrika. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aongoza Kikao kazi cha Shirikisho za Kiuchumi za Afrika.

Addis Ababa, 7 February 2019.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) jana aliendesha kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 
Katika Mwaka 2017. Malaria iliua watu 435,000 duniani, wengi wao wakiwa ni watoto. Asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Africa. Pamoja na kuwa kumekuwa na juhudi kubwa za kutokomeza malaria, Ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kubwa katika juhudi za maendeleo. Ni katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria imeonelea ishirikiane na shirikisho hizo za kikanda kuwa na mikakati ya pamoja katika kutokomeza malaria.
Mhe. Kikwete aliitambulisha rasmi taasisi hiyo ya kutokomeza malaria kwa wajumbe. Taasisi hiyo iliyoanzishwa na Bill Gates pamoja na Ray Cha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More