RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUMIA KONGAMANO LA KUMBUKA MWALIMU NYERERE KUZUNGUMZIA UHURU WA MAWAZO,VIONGOZI KUJISHUSHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUMIA KONGAMANO LA KUMBUKA MWALIMU NYERERE KUZUNGUMZIA UHURU WA MAWAZO,VIONGOZI KUJISHUSHA

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amesema kuna kila sababu ya Watanzania kuendeleza misingi imara iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere huku akisisitiza umuhimu wa watu kuwa huru kutoa mawazo yao badala ya kuyazuia.
Pia ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake licha ya kuwa Rais wa nchini bado hakujali nafasi yake kwani aliamini katika utu na hivyo alikuwa anafikika kwa urahisi na akipenda kujikweza kwa cheo chake kwa kujiona yeye ni Bora au yuko juu zaidi ya Watanzania, siku zote alijishusha na kujiweka kundi la watu wa kawaida sana.
Kikwete ameyasema hayo leo Oktoba 8,mwaka 2019 wakati anafungua Kongamano lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wastaafu na waliopo katika utumishi wamehudhuria .
Wakati Kukwete anazungumza katika kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusisha mchango wa Mwalimu Nyerere katika kujenga mi... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More