RAIS MSTAAFU MKAPA MGENI RASMI KILELE CHA NANENANE KITAIFA 2018 SIMIYU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS MSTAAFU MKAPA MGENI RASMI KILELE CHA NANENANE KITAIFA 2018 SIMIYU

Na Stella Kalinga, Simiyu
RAIS mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa kesho Agosti 08, atakuwa Mgen Rasmi katika Kilele cha Maonesho ya Sherehe ya wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2018, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Akizungumza na vyombo vya habari , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkapa atakuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Amesema pia katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho hayo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watashiriki wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM , Dkt. Bashiru Ally Sambamba na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali.
“Watakuwepo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali za Fedha wakiwemo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Prof. Florens Luoga na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi”Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu , Bw. Jumanne Sagini(kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akitoa maelezo ya awali kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (kulia) wakiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Source: Issa MichuziRead More