Rais Museveni awasili Tanzania  - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais Museveni awasili Tanzania 

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewasili Tanzania kwa ziara ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli kisha wawili hao kuongozana hadi Ikulu jijini Dar es salaam.Rais Museveni amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa 3:45 asubuhi ya leo kisha kupokelewa kwa ngoma za asili na kusalimiana na maofisa wa Serikali wa hapa nchini.


Viongozi hao watakuwa na majadiliano ya faragha Ikulu jijini Dar es salaam kisha kuzungumza na waandishi wa habari kabla Rais huyo wa Uganda hajarejea nyumbani.


The post Rais Museveni awasili Tanzania  appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More