RAIS MUSEVENI WA UGANDA KUTUA KESHO KWA RAIS DKT. MAGUFULI CHATO - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS MUSEVENI WA UGANDA KUTUA KESHO KWA RAIS DKT. MAGUFULI CHATO

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kesho Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019 atafanya Ziara Binafsi ya siku 1 moja hapa nchini.
Mhe. Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Akiwa Chato, Mhe. Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli.
Gerson MsigwaMkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULUChato12 Julai, 2019
Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG


Source: KajunasonRead More