RAIS SHEIN AFUNGA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA , AIPIGIA DEBE LUGHA YA KISWAHILI NCHI ZA SADC - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS SHEIN AFUNGA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA , AIPIGIA DEBE LUGHA YA KISWAHILI NCHI ZA SADC

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amefunga rasmi Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuna kila sababu ya kuifanya lugha ya Kiswahili iwe ya kuwaunganisha wanachama wa jumuiya hiyo.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho hayo pamoja na kuelezea kufurahishwa na namna ambavyo yamefana ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa nchi za jumuiya hiyo kuendelea kusaidiana na kujengeana uwezo ili kuhakikisha wanafikia malengo ya maendeleo na hasa kupitia viwanda.
“Tunaweza kuongeza masoko na ajira kwa kupenda vya kwetu ambavyo vinazalishwa kwenye nchi za jumuiya yetu na ukweli ni chako ni chako na cha mwenzio sio chako. Hivyo umefika wakati wa kupenda bidhaa ambazo zinazalishwa na nchi wanachama wa jumuiya hiyo,”amesema Rais Shein.
Pia ametumia nafasi hiyo kueleza kuna kila sababu ya kuongeza ubora wa bidhaa ili kuvutia wanunuzi wengi z... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More