Rais wa Uturuki Recep Erdogan aeleza A-Z kifo cha mwandishi Khashoggi ‘ubalozi wa Saudi Arabia uliharibu kamera kabla ya kumuua’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais wa Uturuki Recep Erdogan aeleza A-Z kifo cha mwandishi Khashoggi ‘ubalozi wa Saudi Arabia uliharibu kamera kabla ya kumuua’

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan leo Alasiri amehutubia Bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza juu ya kifo cha Mwandishi wa Habari Jamal Khashoggi aliyeuawa ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia Mjini Instabul mnamo Oktoba 02, 2018.


Image result for recep erdogan vs jamalRais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan

Erdogan amesema kuwa kifo cha  mwandishi huyo kilipangwa na Maafisa wa Saudi Arabia nchini Uturuki na sio kuwa kilitokea kwa bahati mbaya kama serikali ya nchi hiyo ilivyoripoti awali.


Akihutubia kwa hudhuni, Erdogan amesema kuwa siku moja kabla ya kifo cha Khashoggi, maafisa usalama 15 wa Saudi Arabia walijipanga makundi matatu Mjini Instabul ambapo watu 9 waliweka kambi katika msitu wa Belgrad uliopo kilometa 55 kusini mwa Instabul.


Erdogan amesema masaa machache kabla ya Khashoggi kuingia kwenye Ofisi za ubalozi huo kamera za usalama zilizimwa.


Tumeshawambia kuwa tutaweka ukweli wote hadharani, hatuwezi kunyamaza juu ya tukio hili. Tunaahidi kuchukua hatua zote muhimu hadi kuhahakisha kuwa haki imetendeka,“am... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More