Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ataka uchunguzi ufanyike ndani ya ubalozi wa Saudia jijini Istanbul kuhusu kupotea kwa Mwandishi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ataka uchunguzi ufanyike ndani ya ubalozi wa Saudia jijini Istanbul kuhusu kupotea kwa Mwandishi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameitaka Saudia kutoa ushahidi kuhusiana na mwandishi wa habari aliyepotea kwamba alitoka nje ya majengo ya ubalozi wao mjini Istanbul.Mwandishi huyo raia wa Saudia Jamal Khashoggi kwa mara ya mwisho alionekana katika jengo hilo la ubalozi wiki iliyopita.Hapo jana Rais Trump alielezea kusikitishwa kwake kutokana na kutoweka kwa mwandishi huyo.


Uturuki imeomba kufanya uchunguzi ndani ya majengo hayo ya ubalozi,kwa madai kuwa Khashoggi aliuawa ndani ya majengo hayo kwa mjibu wa taarifa za vyombo vya habari.Siku ya jumapili wachunguzi kutoka Uturuki walisema wana uhakika kuhusiana na kuuawa kwa mwandishi huyo na kwamba aliuawa na watu 15 kutoka Saudia ambao wanadaiwa waliingia nchini humo wiki iliyopita.


Hakuna ushahidi uliowasilishwa.Mwana Mfalme Mohammed bin Salman awali alisema maofisa wa uchunguzi wanaruhusiwa kuingia katika majengo ya ubalozi wao nchini humo kupeleleza akisistiza hakuna jambo baya lililotendeka.Khashoggi alikuwa akiishi Mare... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More