RAIS WA ZAMANI WA ZFA NA CECAFA ALI FEREJ TAMIM AFARIKI DUNIA LEO ZANZIBAR - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS WA ZAMANI WA ZFA NA CECAFA ALI FEREJ TAMIM AFARIKI DUNIA LEO ZANZIBAR

Na Salum Vuai ZANZIBAR
ALIYEWAHI kuwa Rais wa muda mrefu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA-Sasa ZFF) Ali Ferej Tamim, amefariki dunia leo mjini Zanzibar. 
Marehemu Ferej aliyeiongoza ZFA kwa zaidi ya miaka 20 tangu, amekutwa na mauti baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazimika kufanyiwa upasuaji nchini India mapema mwaka jana.
Katika kipindi cha uongozi wake ZFA, alishiriki kikamilifu katika jitihada za kuiombea Zanzibar uanachama wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) tangu lilipokuwa chini ya urais wa Joao Havellenge.

Aidha, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na baada ya  kustaafu alikuwa mjumbe wa heshima katika baraza hilo.
Ferej aliyefariki akiwa na umri wa miaka 67, alizaliwa tarehe 27 Oktoba, 1952 mjini Zanzibar, na aliichezea klabu kongwe ya Malindi SC na baadae kuwa kocha wa timu hiyo kwa miaka kadhaa.
Akishirikiana na wasaidizi wake, aliisaidia Zanzibar kupata uanachama shirikishi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) inaoendelea nao ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More