RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI MPYA WA PALESTINE NA UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA NCHINI NORWAY. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI MPYA WA PALESTINE NA UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA NCHINI NORWAY.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema misaada mbali mbali iliyotolewa na Chuo Kikuu ‘Houkeland University Hospital’, imekwenda sambamba na dhamira ya muda mrefu ya Serikali ya kutoa huduma bora za tiba ya akili kwa wananchi wake.

Dk. Shein amesema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, alipozungumza na ujumbe wa Madaktari wanne kutoka chuo kikuu cha ‘Houkeland University Hospital’ cha nchini Norway, ukiongozwa na Katibu Mtendaji Eivind Hamsen. Alisema kwa nyakati tofauti Serikali kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo imekuwa ikifanya kila juhudi kuhakikisha inaimarisha upatikanaji wa huduma za tiba ya akili katika Hospitali yake iliopo Kidongochekundu mjini hapa na kuondokana na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa eneo hilo ni ‘jela’ ya wagonjwa hao.

“Serikali imekuwa ikifanya kila juhudi kuimarisha Hospita hiyo, ili ionekane ni kituo cha tiba ya akili, sio tena jela ya wendawazimu kama ilivyokuwa ikitambul... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More