RAJA WATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO LICHA YA KUPIGWA 3-1 NA AS VITA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RAJA WATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO LICHA YA KUPIGWA 3-1 NA AS VITA

TIMU ya Raja Casablanca ya Morocco imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana licha ya kichapo cha mabao 3-1 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji, AS Vita Club.
Kwa matokeo hayo, Raja wanabeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya awali kushinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Casablanca. 
Na ushindi huo unamaanisha vigogo hao wa Morocco wamemaliza ukame wa miaka 15 wa kusbiri taji la Afrika, tangu walipotwaa Kombe la CAF mwaka 2003.

Hilo linakuwa taji la sita la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa Wamorocco hao, ambao tayari wametwaa mataji mengine kama Ligi ya Mabingwa mara tatu na Super Cup mara moja. 
Abdelilah Hafidi aliifungia Raja bao la kuongoza dakika ya 21 kwa ustadi wa hali ya juu mbele ya mashabiki 80,000 waliojitokeza Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa.
Bao lilimaanisha Vita Club ambao taji lao pekee la CAF walilichukua miaka 45 iliyopita, walihitaji kufunga mabao matano ili wabebe taji hilo.
Jean-Marc Mak... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More