Rashford amepewa u “legend” akiwa bado kijana, tuwaone malegend wenzake United - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rashford amepewa u “legend” akiwa bado kijana, tuwaone malegend wenzake United

Tangu apewe nafasi katika kikosi cha kwanza na kocha Louis Van Gaal, kinda wa Manchester United Marcus Rashford amekuwa akikua siku hadi siku na kadri muda unavyokwenda amekuwa akiaminiwa United.


Pamoja na kutopata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha United lakini kitendo cha Rashford kupewa jezi namba 10 kinaonesha imani kubwa ya United kwa kinda huyo, na leo tuone baadhi ya “malegend” ambao wamewahi kuvaa uzi Rashford aliopewa.


George Best. Best alitamba zaidi akiwa na jezi namnmba 7 akiwa United lakini aliwahi kuvaa 8, 10 na 11. Mwaka 1972 ndio aliondoka United akiwa na miaka 27 tu na wakati anaondoka alikuwa akivaa jezi namba 10.Ruud Van Niestrooy. Mwizi wa magoli Manchester United, Mholanzi huyu ni kati ya namba 10 ambazo hazisahauliki United. Huyu alisainiwa kwanza mwaka 2000 lakini kutokana na majeraha akawa nje na ilipofika 2001 akarudi tena.


Msimu wa kwanza tu akapiga mabao 36 katika michezo 49, akafunga mabao 10 katika Champions League na kuibuka mfungaji bora, kiujumla Niestrooy amefunga mabao 150 katika mechi 210 United.Wayne Rooney. Wazza 10 hii ndio namba 10 ya mwisho iliyoondoka United ambayo watu waliipenda sana, uwezo wa Rooney na kujituma kwake kwa United vilimfanya awe katika roho za mashabiki wa Manchester United.


Rooney amedumu Manchester United kwa misimu 11 na katika misimu hiyo alifunga jumla ya mabao 197 katika mechi 396 kabla ya kutimkia katika klabu yake ya utotoni klabu ya Everton.Zlatan Ibrahimovich. Muda mfupi tu aliokaa Manchester United alifanya kazi ambayo kila mshabiki wa United hakutaka aondoke, Zlatan alifanikiwa kucheza mechi 28 tu kwa Manchester United huku akifunga mabao 17, majeraha yakamuondoa United.Tedd Sherigham. United walimnunua kutoka Tottenham mwaka 1997, kuanzia 1997 hadi 2001 Sherigham alicheza michezo 104 United akifunga jumla ya mabao 31, alikuwepo msimu wa mwaka 1999 wakati United wakibeba makombe 3 makubwa(FA,EPL na Champions League)


Source: Shaffih DaudaRead More