Rasmi Cristiano Ronaldo ajiunga na Juventus ya Italia - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rasmi Cristiano Ronaldo ajiunga na Juventus ya Italia

Klabu ya Real Madrid imethibitisha mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo amejiunga na Juventus ya nchini Italia.Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka hivi punde klabu hizo mbili zimeafikiana malipo ya pauni milioni 105 kwaajili ya nahodha huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33.


Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or ametumia misimu tisa Madrid baada ya uhamisho wake wa pauni milioni 80 akitokea Manchester United huku akiondoka na kuwacha rekodi ndani ya klabu hiyo kwa kufunga jumla ya mabao 451.


Nahodha huyo wa Ureno anaondoka Real baada ya kushinda mataji mawili ya La Liga titles, mawili Copa del Rey na mataji manne ya klabu bingwa barani Ulaya.


The post Rasmi Cristiano Ronaldo ajiunga na Juventus ya Italia appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More