RASMI, KUANZIA LEO OKTOBA 8, 2018 MASOUD JUMA IRAMBONA SI KOCHA WA SIMBA SC TENA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RASMI, KUANZIA LEO OKTOBA 8, 2018 MASOUD JUMA IRAMBONA SI KOCHA WA SIMBA SC TENA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
HATIMAYE klabu ya Simba SC leo imetoa tamko rasmi la kuachana na Kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Juma Irambona baada ya takriban mwaka mmoja wa kuwa klabu.
Kaimu Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema kwamba uamuzi huo ni kwa faida ya klabu na kwa maslahi ya pande zote mbili na kumshukuru kocha huyo kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi chote alichofanya kazi Msimbazi na kumtakia kheri katika maisha yake mapya nje ya klabu hiyo.
“Tumekaa naye vizuri, ametusaidia sana, lakini kila jambo lina mwisho wake, kwa faida ya klabu yetu tumefikia makubaliano kwa faida ya pande zote mbili kuuvunja mkataba huu, ili tuweze kuendelea. Tumemfungulia mlango Masoud kwa roho safi, na huenda hii ikawa ni bahati yake huko mbele ya safari kwa sababu tunaamini ni mwalimu mzuri,” amesema taarifa hiyo. 
Lakini Abdallah amesema kwamba japo anaamoini Juma atapata klabu nyingine kubwa zaidi, lakini Mungu akipenda anaweza kurudi Tanzania kufundisha Simba SC.
Kwa upande ... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More