RASMI TFF ‘YAMTUPIA VIRAGO’ AMUNIKE BAADA YA TAIFA STARS KUBORONGA AFCON - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RASMI TFF ‘YAMTUPIA VIRAGO’ AMUNIKE BAADA YA TAIFA STARS KUBORONGA AFCON

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemfuta kazi kocha Mnigeria wa timu ya taifa, Emmanuel Amunike baada ya Taifa Stars kufanya vibaya kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Misri kufuatia kufungwa mechi zote tatu za Kundi C.
Taarifa ya TFF leo imesema kwamba wamefikia makubaliano ya pamoja na Amunike kusitisha mkataba baina yao.
Aidha, TFF imesema kwamba itatangaza Kocha wa muda atakayekiongoza Taifa Stars katika mechi za kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.

Baada ya kufungwa 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria, Taifa Stars iliondoka Misri bila hata pointi moja, ikishika mkia kwenye Kundi C, nyuma ya jirani zao, Kenya waliovuna pointi tatu, huku Senegal iliyomaliza na pointi sita katika nafasi ya pili ikiungana na Algeria iliyokusanya pointi tisa kwenda hatua ya 16 Bora.
Taifa Stars ya kocha Emmanuel Amunike imeshindwa kuvunja r... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More