Rayvanny awavimbia BASATA, apingana na amri ya kufuta wimbo wake wa ‘Mwanza’ mitandaoni - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rayvanny awavimbia BASATA, apingana na amri ya kufuta wimbo wake wa ‘Mwanza’ mitandaoni

Licha ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kumtaka Rayvanny aufute wimbo wake mpya wa Mwanza kwenye mitandao ya kijamii kabla ya saa 10:00 jioni ya leo,  Msanii huyo mpaka sasa hajaufuta wimbo huo mtandaoni.Video ya wimbo huo mpaka sasa umetazamwa mara milioni 1+ (views milioni 1+) na kwa Tanzania upo namba moja kwenye Trending katika Mtandao wa YouTube.


Mapema leo BASATA walitoa tamko la kuufungia wimbo huo kutotumika kwa namna yoyote ile kwa kile walichoeleza kuwa maudhui ya wimbo huo yanakiuka maadili ya mtanzania.


SOMA ZAIDI-BASATA wamtaka Rayvanny na Diamond kuuondoa wimbo Mwanza mtandaoni, watishia kufungia Wasafi Festival (Video)
The post Rayvanny awavimbia BASATA, apingana na amri ya kufuta wimbo wake wa ‘Mwanza’ mitandaoni appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More