RC CHALAMILA AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MBEYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC CHALAMILA AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MBEYA

Na Emanuel Madafa, Mbeya .Dhamira ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwapatia wananchi huduma nzuri, itafanikiwa endapo viongozi wenye dhamana ya kuisimamia Serikali hawatakuwa wasanii wa kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya inayojengwa Inyala kwa gharama ya Sh1.5 bilioni na kuonekana kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.
Chalamila amesema Rais Magufuli ana nia njema kwa Watanzania lakini baadhi ya wasaidizi wake ndio wanaomuangusha na ndio sababu inayomfanya kupangua pangua safu ya uongozi wake.
Amesema endapo viongozi walioaminiwa wakiwa ni wasanii katika kusimamia na kutekeleza maazimio ya Rais Magufuli hawatakuwa wamembeba wala kumuwakilisha vyema.
“Tukiacha usanii na kuweka kando rushwa na ufisadi…tutakuwa tumembeba vizuri Rais katika kuwatumia Watanzania.  Kwa hiyo hospitali hizi zote za mkoa wetu wa Mbeya zinaenda vizuri sana na hii inadhihirisha sisi viongo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More