RC CHALAMILA-MARUFUKU KUJIITA RAIS MBEYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC CHALAMILA-MARUFUKU KUJIITA RAIS MBEYA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema ni marufuku mtu yeyote tofauti na Rais Dk. John Magufuli kujiita Rais au kiongozi yeyote kuingilia madaraka ya mwingine katika mkoa huo na kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba, sheria na taratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari Chalamila amesema upo mtindo wa baadhi ya wabunge kujiita marais na kwamba kufanya hivyo ni kosa kwani mbunge hawezi kuwa Rais na wala hawezi kufanya majukumu ya Rais.
Anasema ni vyema watu wajitambue na kila kiongozi kumiliki majukumu yake pasipo kuingilia nafasi au mhimili mwingine wa dola ili kuepusha migongano na mifarakano katika utendaji kazi wao.
“Nimesema watu wajitambue, ni marufuku wewe mbunge kujiita Rais kwasababu Rais ni Mhimili mwingine. Ni marufuku mimi mkuu wa mkoa kujiita Mbunge, ni marufuku mtendaji wa mtaa kujiita mtendaji wa kata au wa kata kujiita wa mtaa, kila mtu amiliki majukumu yake,” anasema na kusisitiza.
“Rais ni mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More